Job Search

NAFASI ZA KAZI
Nafasi: Mshauri wa Biashara(20)
Program: Uimarishaji wa Maendeleo ya vijana vijijini kupitia Biashara (STRYDE 2.0)
Eneo: Wilaya za Mbozi, Kyela
TechnoServe ni Shirika la Maendeleo, la Kimataifa na lisilo la kifaida. Lengo lake kuu ni kufanya
kazi na watu wanaojishughulisha na biashara na wenye mtazamo wa kibiashara/kijasiriamali
katika nchi zinazoendelea ili kujenga ushindani katika kilimo, ufugaji, biashara na viwanda.
TechnoServe tunaamini suluhisho la kupunguza umaskini ni kuendeleza biashara kwa
kuwaunganisha watu na taarifa sahihi, mitaji na masoko.
Kazi zetu zimejikita katika kutambua fursa nzuri za biashara zinazoweza kuchangia uchumi na
kuleta matokeo chanya kwa watu maskini waliopo vijijini. Mbinu yetu ni kuajiri watu wenye
utendaji na ufanisi wa hali ya juu ambao hushiriki Dira yetu ya sekta binafsi katika kutengeneza
ufumbuzi endelevu kwa umaskini.Tunaamini katika kufanya kazi kwa bidii na ubunifu.Kwa sasa
tunafanya kazi katika zaidi ya nchi 30 barani Afrika, Latini ya Amerika na Asia.
MADHUMUNI
Kutoa usaidizi wa moja kwa moja kwa vijana kupitia shughuli mbalimbali za Mradi wa Uimarishaji
wa maendeleo ya vijana vijijini kupitia Biashara (STRYDE 2.0) katika nchi ya Tanzania ndani wilaya
5 za mkoa wa Mbeya. Mshauri Biashara atafanya kazi kwa karibu na jamii zilizopo vijijini, vijana,
wadau mbalimbali na viongozi wasimamizi wa shirika la TechnoServe.
Atakuwa na jukumu la utekelezaji wa shughuli za mradi kwa wakati na kwa ufanisi sambamba na
kufanikisha kufikia malengo ya Mradi ya kuwezesha vijana wapatao 15,400 walioko vijijini ili
kuongeza ushiriki wao katika uzalishaji uchumi nchini Tanzania. Atawajibika pia katika
kutengeneza mpango kazi wake, kutoa mafunzo kwa vijana, kusimamia shindano la mpango
biashara katika ngazi ya wilaya, kata au kijiji, kutoa ushauri wa biashara kwa wajasiriamali vijana
na kufanya ufuatiliaji wa matokeo na ufanisi wa mradi kwa kijana mmoja mmoja. Mshauri
biashara pia atatakiwa kutoa taarifa za mara kwa mara juu ya maendeleo ya shughuli za mradi.
WAJIBU NA MAJUKUMU
Uhamasishaji wa washiriki vijana kujiunga na Mradi wa STRYDE
o Kuutangaza Mradi na faida zake ndani ya jamii katika eneo mradi.
o Kuwatambua na kuwasajili washiriki vijana ambao wamekidhi vigezo vya mradi
ambavyo ni umri, uwezo wa kusoma na kuandika na eneo la mradi.
o Kuwezesha utambulisho wa vikundi na kufanya mazoezi yanayojenga timu bora
ili kuimarisha mahusiano ndani ya vikundi, na kusaidia katika utafutaji wa
ukumbi/darasa sahihi ndani ya eneo la mradi.
o Kuwa mwakilishi mzuri wa shirika na mradi kulingana na sera ya shirika.
Kutoa Mafunzo na kusimamia washiriki wa STRYDE wasikatishe ushiriki :
o Kuhudhuria mafunzo ya kuongeza uwezo na ujuzi juu ya mtaala unaotumika
katika mradi kama inavyotakiwa (Kushiriki mafunzo ya uwezeshaji kwa
wawezeshaji)
o Kufundisha mtaala unaotumika katika mradi kama inavyotakiwa, kufuatia
miongozo na viwango vya kuzingatia muda, ukubwa wa darasa, matumizi ya zana
za kufundishia, mazoezi, andalio la somo na kuhakikisha kwamba mafunzo
yanaendeshwa kama mradi unavyotaka kwa mfumo wa awamu(cohort).
o Kuhakikisha kuwa utoaji wa mafunzo ni wa ubora wa hali ya juu, ni sahihi kwa
mazingira ya maeneo husika na kwa kutumia lugha ya eneo husika na yanawafikia
walengwa kwa ufanisi.
o Kutambua ujuzi unaohitajika ndani ya makundi ya STRYDE unaoendana na fursa
za kiuchumi zilizopo kwenye maeneo yao na kutoa mrejesho kwa msimamizi
wake aina ya mafunzo inayohitajika kupata ujuzi huo.
o Kufuatilia na kuhakiki mahudhurio ya washiriki na kutoa taarifa juu washiriki
wanaokatisha mafunzo na changamoto nyingine zinazojitokeza, kwa msimamizi
wao mara kwa mara.
o Kuweka juhudi katika ufuatiliaji na kutoa usaidizi kwa washiriki wa STRYDE
ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile matatizo ya kijinsia,
mahusiano, Kisaikolojia, kushuka kwa mahudhurio ya Vijana n.k
o Kuhakikisha anazingatia muda na ubora katika utekelezaji wa shughuli za mradi.
Kutoa Usaidizi kwa washiriki wakati wa kipindi cha Malezi na uangalizi na kuripoti kwa
mshauri biashara mwandamizi.
o Kuwafuatilia vijana baada ya mafunzo kuangalia maendeleo yao kwa mfano
walipata ajira, walioanza biashara au shughuli nyingine. Kuwapatia ushauri,
mwongozo na msaada mwingine wowote kadri inavyohitajika.
o Akishirikiana na washauri biashara wengine wa eneo husika, ataratibu na
kusimamia shindano la mpango biashara katika ngazi ya wilaya/kata na kutoa
usaidizi katika zoezi la kuandaa na kuwasilisha mpango biashara.
o Kufuatilia, kukusanya na kuripoti na kushirikisha timu kuhusu mafanikio na
changamoto zinazojitokea katika utekelezaji wa mradi.
o Kutoa ushauri kwa wajasiriamali vijana wa vijijini ili kutekeleza mipango biashara
yao ikiwemo kuanzisha na kukuza biashara zao.
o Kutoa usaidizi kwa Meneja Ushirikiano na Mahusiano(CPM) katika utekelezaji
shughuli za kipindi cha malezi na uangalizi.
o Kutoa usaidizi katika utambuzi na kupendekeza washiriki wazuri
watakaowakilisha vijana katika Baraza la Ushauri la vijana katika maeneo yao.
o Kufanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali walioko kwenye maeneo yao na
kuhakikisha wana uelewa sahihi juu ya mradi na utekelezaji wake.
o Kuwatambua wadau mbali mbali ambao watashirikiana na vijana katika mradi na
kufungua fursa za mafunzo ya ujuzi na ajira.
o Kushiriki kikamilifu katika mikutano ya kawaida ya timu ya kufuatilia maendeleo
ya utekelezaji wa mradi na kushirikisha taarifa (data) za eneo husika (mfano;
orodha ya mahudhurio ,maoni, fomu nk.)
o Kuwatambua vijana na viongozi watakaounda kamati ya ushauri ya STRYDE.
o Kukusanya taarifa za ufatiliaji na tathmini kwa wakati na kuziwakilisha kulingana
na matakwa ya mtKutekeleza kazi nyingine zozote anazopewa na msimamizi
wake/msimamizi wa mradi.
Mwombaji lazima awe na Vigezo vifuatavyo.
o Elimu ngazi ya Stashahadaau Cheti katika masuala ya Biashara, Elimu, Kilimo,
Maendeleo ya Jamii na fani nyingine zinazoendana na hizo kutoka katika vyuo
vinavyotambulika na serikali.
o Awe na Uzoefu wa MWAKA MMOJA kwenye sekta ya Uwezeshaji/Ufundishaji
vijana, katika fani za Maendeleo ya Jamii, Miradi ya Ujasiriamali/Biashara au
Ufundishaji wa Mafunzo ya Ujuzi.
o Uwezo wa kuongea na kuandika vizuri lugha ya Kiingerezana Kiswahili. (Lugha ya
eneo husika hususani lugha za mkoa wa Mbeya ni sifa ya ziada)
o Uzoefu wa kufanya kazi na kutoa mafunzo na ushauri kwa vijana.
o Hamasa ya ujasiriamali, Uzoefu katika shughuli za kijasiriamali/biashara na kilimo
ni sifa ya ziada.
o Uwezo wa kufanya kazi chini ya uangalizi mdogo na kutatua matatizo katika
mazingira ya kazi.
o Utayari wa kufanya kazi katika mazingira ya vijijini
o WAKAZI WA MAENEO HUSIKA (KYELA NA MBOZI) WATAPEWA KIPAUMBELE.
Tuma maombi yako kwa:
MenejaRasilimali Watu, (Human Resource Manager) TechnoServe P.O.Box 78375 Dar es Salaam,
Unaweza pia kufikisha maombi yako;
Ofisi zetu zilizopo Kabwe kwenye Jengo la Kisangani (NMB bank) ghorofa ya tatu,
Ofisi zetu zilizopo Kyela kwenye Jengo la Benki CRDB.
Au kupitia barua pepe tz-info@tns.org
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 08 Julai, 2016.

0 comments:

Post a Comment